Muongozo / zana ya sauti ya pamoja katika kuimarisha ustahimilivu wa mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi
Toolkit, 80 pages

Zana ya Sauti ya Pamoja inatoa mbinu rahisi na yenye gharama nafuu katika kubainisha vipaumbele vya wanawake na vijana katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi kwa kutumia njia shirikishi. Zana hii imetengenezwa ili iweze kutumiwa na serikali za mitaa, mashirika/taasisi za kijamii zenye malengo ya kutaka kuelewa, kuwakilisha na kujumuisha vipaumbele katika kupanga mipango ya maendeleo.