17501IIED.pdf
Language:
English, Swahili
Published: January 2007
Area(s):
Natural Resource Issues
ISBN: 9781843697237
Product code:13543IIED

Watu maskini wanategemea kwa kiwango kikubwa Mazingira na rasilimali zake kama maji safi na ardhi yenye rutuba. Aidha, wao ni wahanga wakubwa wa majanga yatokanayo na uharibifu wa mazingira. Hali kadhalika ukuaji wa uchumi pia hutegemea maliasili na mazingira. Hivyo ni muhimu kujumuisha masuala ya Mazingira katika mchakato wa Mipango na maendeleo. Tathmini ya awali inaonesha suala la Mazingira halijapewa kipaumbele katika mikakati mingi ya kupambana na umaskini inayoandaliwa na nchi mbalimbali. Je ukweli ni upi, na lipi laweza kufanyika juu ya jambo hili? Waandishi wa Kitabu hiki wameonesha jinsi Tanzania ilivyoweza kufanikisha jambo hili, wadau, juhudi mbali mbali zilizofanyika, matukio na uzoefu uliopatikana katika kujumuisha Masuala ya Mazingira katika mchakato wa kupambana na Umaskini. Mafanikio mengi yametokana na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA) ambao uliwezesha kujumuisha masuala ya Mazingira. Waandishi wameelezea kwa undani mchakato huu,mafanikio yake, changamoto na kutoa mwongozo kwa nchi nyingine zinazokusudia kujifunza.

Cite this publication

Assey, P., Bass, S., Cheche, B., Howlett, D., Jambiya, G., Kikula, I., Likwelile, S., Manyama, A., Mugurusi, E., Muheto, R. and Rutasitara, L. (2007). Mazingira ni Kitovu Cha Maendeleo Tanzania. .
Available at https://www.iied.org/sw/17501iied