iied
iied

Publications

Browse themes
About publications

Information for 17501IIED

Mazingira ni Kitovu Cha Maendeleo Tanzania

Watu maskini wanategemea kwa kiwango kikubwa Mazingira
na rasilimali zake kama maji safi na ardhi yenye rutuba. Aidha,
wao ni wahanga wakubwa wa majanga yatokanayo na uharibifu
wa mazingira. Hali kadhalika ukuaji wa uchumi pia hutegemea
maliasili na mazingira. Hivyo ni muhimu kujumuisha masuala ya
Mazingira katika mchakato wa Mipango na maendeleo. Tathmini ya
awali inaonesha suala la Mazingira halijapewa kipaumbele katika
mikakati mingi ya kupambana na umaskini inayoandaliwa na nchi
mbalimbali. Je ukweli ni upi, na lipi laweza kufanyika juu ya jambo hili?
Waandishi wa Kitabu hiki wameonesha jinsi Tanzania ilivyoweza
kufanikisha jambo hili, wadau, juhudi mbali mbali zilizofanyika,
matukio na uzoefu uliopatikana katika kujumuisha Masuala ya
Mazingira katika mchakato wa kupambana na Umaskini. Mafanikio
mengi yametokana na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza
Umaskini (MKUKUTA) ambao uliwezesha kujumuisha masuala
ya Mazingira. Waandishi wameelezea kwa undani mchakato
huu,mafanikio yake, changamoto na kutoa mwongozo kwa nchi
nyingine zinazokusudia kujifunza.

Publication information

Download and Sharing

Free PDF 602k

Share with your network:

Match 1 / 6
See all      Close<>
We use cookies to help improve this website. Clicking any link on this site will be taken as your consent to this.